BOIPLUS SPORTS BLOG

SHANGHAI,China
MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Chelsea Demba Ba anayekipiga Shanghai Shenhua inayoshiriki ligi kuu ya China amevunjika mguu katika mchezo wa 'Shanghai Derby' dhidi ya Shanghai SIPG FC.

Ba tayari ameshafunga magoli 14 katika michezo 18 aliyoteremka dimbani na amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho.

Msenegal huyo alitolewa uwanjani dakika ya 70 baada ya kuumizwa vibaya na beki wa SIPG ambapo inaonekana anaweza akakaa nje kwa muda mrefu kulingana na ripoti ya daktari.


Licha ya kuumia kwa mshambuliaji huyo lakini Shenhua iliibuka na ushindi wa magoli 2-1 huku goli la pili likifungwa kwa mkwaju wa penalti na kiungo Fredy Guarin.

Shenhua ni miongoni mwa timu zinazolipa fedha nyingi wachezaji wake ambayo pia iliwahi kumsajili mshambuliaji raia wa Cameroon Samuel Eto'o miaka minne iliyopita.

Tayari wachezaji wa timu hiyo wameshaandika katika mitandao ya Twitter kumtakia kheri mshambuliaji huyo.

Post a Comment

 
Top