BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK, Ubelgiji
KIKOSI cha timu ya KRC Genk ambacho anachezea mshambuliaji Mtanzania Mbwana Samatta kimesafiri leo hii kuelekea nchini Montenegro kwa ajili ya mchezo wa marudiano michuano ya Europa ligi dhidi ya Budućnost.

Katika mchezo wa awali Genk iliibuka na ushindi wa magoli 2-0 ambapo Samatta alifunga goli la pili na kusaidia miamba hiyo ya nchini Ubelgiji kutoka kifua mbele katika uwanja wa nyumbani.

Genk inahitaji sare yoyote au kupoteza kwa goli moja kwa ajili ya kufuzu katika hatua inayofuata ya michuano hiyo ambayo inafuatiliwa na mamilioni kote ulimwenguni.

Endapo Genk itafuzu hatua hiyo itakuwa ni nafasi ya Samatta kuonekana na klabu kubwa kwakuwa ataweza kucheza dhidi ya timu kubwa kama Manchester United, Tottenham Hotspur na nyinginezo.

Tangu kujiunga kwa Samatta na miamba hiyo akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia Kongo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu.

Post a Comment

 
Top