BOIPLUS SPORTS BLOG

TURIN,Italia
MSHAMBULIAJI wa Napoli Gonzalo Higuain amefanyiwa vipimo vya afya tayari kujiunga na Juventus kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufika pauni 94.7 milioni.

Maofisa wa Juventus walikutana na wakala wa mchezaji huyo raia wa Argentina nchini Hispania  ili kukamilisha dili hilo wikiendi hii.

Higuain mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na timu kadhaa barani Ulaya zikiwemo Arsenal na Paris Saint German.

Higuain amefunga magoli 36 msimu uliopita katika Seria A kitu kilichowavutia mabosi wa vibibi vizee vya Turin.

Juve wamempoteza mshambuliaji wao Alvaro Moratta aliyejiunga na Real Madrid huku kiungo Paul Pogba akijiandaa kuhamia Manchester United lakini tayari imewasajili Dani Alves pamoja Miran Pjanic.

Post a Comment

 
Top