BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
KOCHA mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili, Taifa Stars ina pointi moja wakati Chad ilijitoa katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.

Kikosi hicho kitakachoingia kambini kuanzia Agosti 1-5 kina wachezaji wafuatao;

Walinda Mlango:
Deogratius Munishi, Aishi Manula, Benno Kakolanya.

Walinzi:
 Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Mohamed Hussein, Juma Abdul, Erasto Nyoni.

Viungo:
Himid Mao, Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Ibrahim Jeba, Mwinyi Kazimoto, Farid Mussa, Hassan Kabunda, Simon Msuva.

Washambuliaji:
 Joseph Mahundi, Jamal Mnyate, Ibrahim Hajib, John Bocco, na Jeremiah Juma.

Post a Comment

 
Top