BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu, Dar
KAMATI ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imemfungia mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na faini ya Sh. Milioni 3.

Kamati hiyo iliyokaa jana Julai 7 chini wa Mwenyekiti Wakili Wilson Ogunde imemkuta Jerry akiwa na makosa matatu yaliyowasilishwa kwao.

Kosa la kwanza ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa ambapo hajaweza kulipa hadi leo.

Kosa la pili  ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DR Congo.
Katika shitaka hilo, Jerry aliwahamasisha mashabiki wa timu hiyo kukaa pande zote hata ule wa watani wao Simba kitu ambacho kingesababisha uvunjifu wa amani.

Katika shitaka la tatu Muro alifanikiwa kuishinda TFF katika  kupingana na maamuzi ya shirikisho hilo juu ya masuala ya utoaji wa haki za matangazo ya Televisheni.

Licha ya hukumu hiyo Muro ana haki ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya TFF.

Post a Comment

 
Top