BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KATIBU mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameziasa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kutimiza masharti ya kupata vibali vya kuishi na kufanya kazi Tanzania kwa Wataalamu wa kigeni wakiwamo makocha, madaktari na wachezaji kabla ya kusaini nao mikataba.

Masharti hayo ni vibali vya kufanya kazi nchini, visa ya kuishi nchini, vibali vya kucheza mpira wa miguu nchini, vibali vya kufundisha mpira na vibali vya watalaamu wengine kama madaktari na hayo ni kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji na Serikali, lakini wakati huohuo kwa wachezaji nao kukatiwa leseni ya kucheza kutoka TFF.

“Mchezaji au mtaalamu yeyote anapokuja nchini na kuanza mazoezi na timu yoyote atachukuliwa yuko kazini. Tusingependa watu wapate usumbufu. Kama Katibu Mkuu nimepata taarifa kutoka mamlaka zinazohusika kuwa nifuatiulie kl kuwa sisi ndio waratibu wa soka nchini,” alisema Selestine.

“Klabu zihakikishe vyeti vya taaluma vinawasilishwa TFF kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kutiliana kandarasi na ili kujiridhisha na viwango vyao vya elimu katika soka"alisema Mwesigwa.

Wakati huohuo, huo huo TFF imeagiza klabu kuendelea na usajili kabla ya Agosti 6, ambayo itakuwa siku ya mwisho na kwamba hakutakuwa na muda wa kuongezwa kwa timu ambayo itashindwa kukamilisha usajili kwa wakati.

Post a Comment

 
Top