BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda
USIKU wa kuamkia leo nyota  Cristiano Ronaldo alifunga bao moja huku akitengeneza lingine na kuipatia ushindi wa mabao 2-0 timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Wales iliyokuwa ikimtegemea winga Gareth Bale kwenye michuano ya EURO 2016.

Licha ya ushindi huo kuipeleka Ureno katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo, habari ya mjini ni bao la Ronaldo alilofunga baada ya kuruka juu zaidi ya mabeki wa Wales na kuupiga mpira huo kwa kichwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Ronaldo kufunga mabao ya aina hii, mara kadhaa amekuwa akinaswa na kamera akionekana kuwa juu zaidi ya mabeki kiasi kwamba mtu unaweza kujiuliza "Hivi huyu Ronaldo ana injini ya ndege?"

Hizi hapa ni baadhi ya picha zinazomuonyesha mfumania nyavu huyo wa Real Madrid ya Hispania akiwa katika matukio mbalimbali ya aina hii.Post a Comment

 
Top