BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar

BAADA ya kuona uwezekano wa kiungo Justice Majabvi kusalia kikosi msimu ujao ni mdogo, wekundu wa Msimbazi Simba wameamua kusaka jembe la kuziba nafasi yake na sasa wamedondokea kwa Mnyarwanda Imrani Nshimiyimana wa Polisi Rwanda.

Kabla ya kumuibukia kiungo huyo mkabaji anayemudu pia nafasi ya kiungo mshambuliaji, Simba walitaka kumsajili ndugu wa Haruna Niyonzima anayeitwa Muhajili Hakizimana ambaye ni kiungo mshambuliaji, lakini walibadili mawazo baada ya kuona watahitaji mtu katika nafasi ya kiungo mkabaji iliyoachwa wazi na Majabvi.

BOIPLUS ilimtafuta Meneja wa mchezaji huyo, Kazungu Claver ambaye ni mtangazaji maarufu wa vipindi vya michezo kwenye Radio na Luninga nchini Rwanda aliyekiri kuwa kuna mazungumzo yanaendelea huku akisisitiza kuwa bado hayajafikia kiwango cha kuyaweka hadharani.

"Ni kweli wameonyesha nia ya kumsajili na mchezaji yuko tayari kutua Simba muda wowote, ila bado mazungumzo yapo hatua za awali kabisa, mambo yakiwa sawa tutawajuza." alisema Kazungu.


Nshimiyimana ambaye ni mchezaji mrefu na mwenye nguvu amekuwa mhimili mkuu kwenye nafasi ya kiungo ya klabu yake ya Polisi pamoja na timu ya Taifa ya Rwanda, 'Amavubi' na endapo usajili huo utafanikiwa basi atakuwa mchezaji msomi katika klabu ya Simba akiwa na shahada ya Utawala wa Biashara.

Post a Comment

 
Top