BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK,Ubelgiji
MSHAMBULIAJI Mtanzania Mbwana Samatta ameiwezesha timu yake KRC Genk kuibuka na ushindi baada ya kufunga goli la dakika za majeruhi dhidi ya Oostende katika mchezo wa ligi kuu ya Ubelgiji.

Genk imeibuka na ushindi wa magoli 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani  Cristal Arena na kufikisha alama tatu hivyo kuwa na mwanzo mzuri.

Mshambuliaji Niko Karelis ndiye alikuwa wa kwanza kuwapatia wenyeji goli la kuongoza dakika ya 50 baada ya mabeki wa Oostende kuzembea kuondoa hatari langoni kwao.

Samatta aliyetokea benchi alifunga goli la pili dakika ya 90 na kuwahakikishia ushindi wenyeji kabla Knowledge Muso hajafunga goli la kufutia machozi kwa wageni dakika moja baadae.

Post a Comment

 
Top