BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imemsainisha mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic mkataba wa mwaka mmoja toka Paris Saint Germain ya Ufaransa.

Mshambuliaji huyo raia Sweden mwenye miaka 34 amemalizana na mabingwa hao wa Ufaransa na kugoma kuongeza kandarasi mpya badala yake akaamua kujiunga na Mashetani Wekundu.

Ibrahimovic atakuwa akipokea kitita cha 220,000 pauni kwa wiki licha ya kuwa na umri mkubwa ukilinganisha na uwezo wake uwanjani.

Msimu uliopita alimaliza akiwa mfungaji bora wa ligi ya Ufaransa baada ya kufunga magoli 25 .

Huu unakuwa usajili wa pili wa kocha mpya wa United Jose Mourinho baada ya mwezi uliopita kumsajili beki wa kati Erick Bailly toka Villarreal kwa dau la pauni 30 milioni.

Habari ndani ya United zinaeleza kuwa kesho watakamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji toka Borrusia Dortmund Henrick Mikhtarian baada ya kusafiri hii leo toka Ujerumani tayari kufanyiwa vipimo vya afya.

Post a Comment

 
Top