BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga Paul Nonga amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kuwatumikia wachimba madini wa Mwadui ya mkoani Shinyanga kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Nonga ambaye alikuwa na mkataba wa miaka miwili na mabingwa  wa ligi kuu Tanzania bara na kuitumukia kwa mwaka mmoja pekee ameamua kurudi Mwadui ambapo ndiyo Yanga walipomsajili msimu uliopita.

Katibu mkuu wa Mwadui Ramadhani Kilalo ameiambia BOIPLUS kuwa wamemsajili mshambuliaji huyo na tayari amesaini kandarasi lakini alishindwa kuweka wazi kuhusu kiasi cha fedha kutokana na makubaliano yanayoendelea baina ya timu hizo mbili.

"Tumemsajili Nonga toka Yanga na tayari ameshasaini lakini siwezi kuweka wazi kwakuwa makubaliano yanaendelea baina yetu na timu yake ya zamani," alisema Kilalo.

Kwa upande wake Mshambuliaji huyo alisema ameamua kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kuwatumikia wachimba madini hao baada ya kukosa namba ya kudumu katika kikosi cha Yanga.

Mara baada ya kumalizika kwa ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita Nonga aliuandikia barua uongozi wa Yanga kuomba kuuzwa baada ya kukiri kuzidiwa uwezo na washambuliaji Amissi Tambwe na Donald Ngoma.

Kocha wa Mwadui Jamhuri Kihwelo Julio alinukuliwa akisema miongoni wachezaji wenye nidhamu aliowahi kuwafundisha ni Nonga na amefurahi kwa mshambuliaji huyo kurudi tena Mwadui.

Post a Comment

 
Top