BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa

WINGA wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameisaidia timu yake kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya EURO 2016 baada ya kuchangia ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Wales.

Wales walitawala mchezo kipindi cha kwanza lakini hawakufanikiwa kupata goli na hivyo timu hizo kwenda mapumziko zikiwa hazijafungana. 

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Ureno wakionekana kuwa bora zaidi ya Wales hali iliyopelekea kufanikiwa kupata goli katika dakika ya 49 lililofungwa na Ronaldo. 


Dakika tatu tu baada ya bao hilo, Ronaldo alitengeneza goli lingine lililofungwa na Luis Nani katika dakika ya 52 hivyo mchezo huo kumalizika kwa Ureno kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ronaldo ambaye alikua nyota wa mchezo huo ameifikia rekodi ya  Michael Platin ya kufunga goli 9 kwenye michuano hiyo.

Post a Comment

 
Top