BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma,

KAMATI ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limesogeza mbele shauri linalomkabili ofisa Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro kutokana na kukiukwa kwa misingi ya sheria.

Mwenyekiti wa kamati hiyo Wilson Egundu alisema barua aliyotumiwa Jerry ambayo ilimtaka afike mbele yao leo Julai 2 saa 4: 30 asubuhi ina mapungufu kwakua haioneshi alitakiwa kuhojiwa na kamati gani .

"Barua aliyotumiwa ina mapungufu kisheria tunaliagiza shirikisho la mpira wa miguu kuandaa shauri jingine dhidi yake ndiyo aitwe mbele ya kamati" alisema Egundu.

Kwa upande wake Jerry alisema hana kinyongo na viongozi wa shirikisho kwa kutaka kumdhalilisha mbele ya jamii ya mpira lakini ukweli umejulikana baada ya kuonekana hakupaswa kuitwa mbele ya kamati hiyo.

"Huu ni ushindi mwingine tumeupata nje ya uwanja baada ya kuonekana viongozi wa TFF wamejichanganya katika shauri dhidi yangu ila nimewasamehe bure" alisema Jerry.

Shauri hilo lilimtaka ofisa huyo kufika mbele ya kamati hiyo saa 4:30 asubuhi lakini majibu yake yalitolewa saa 10 jioni

Post a Comment

 
Top