BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar

GOLIKIPA wa Coastal Union Fikirini Bakari anatajia kusafiri wikiendi hii kuelekea jijini Mbeya kusaini kandarasi ya kuwatumikia wagonga Nyundo hao timu ya Mbeya City baada ya makubaliano ya pande zote kufanyika.

Firikirini ambaye alikuwa na msimu mzuri licha ya timu yake kushuka daraja atacheza pamoja na golikipa mkongwe Juma Kaseja ambaye yumo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na kocha raia wa Zambia Kinnah Phiri.

Katibu mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe ameiambia BOIPLUS kuwa makubaliano baina yao na mchezaji huyo yanaendelea vizuri na wikiendi hii kipa huyo atasafiri kuelekea jijini Mbeya tayari kusaini kandarasi na Wagonga nyundo hao.

"Ni kweli tumefikia makubaliano na Fikirini na tunatarajia muda wowote kuanzia sasa atakuewepo jijini Mbeya kusaini nasi kwa ajili ya msimu ujao" alisema Kimbe.

Kwa upande wake golikipa huyo ambaye yupo jijini Dar es Salaam amesema wamefikia makubaliano na Mbeya city na kuna uwezekano mkubwa wa kuvaa jezi za zambarau msimu ujao.

"Nimeongea nao na tumefikia makubaliano mazuri muda si mrefu kila kitu kitakuwa wazi" alisema Fikirini.

BOIPLUS iliwatafuta viongozi wa Wagosi wa kaya lakini hakuna aliyepatikana kuzungumzia suala hilo.

Post a Comment

 
Top