BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda

 Kiongera akishangilia bao lake dhidi ya Thiker UnitedKILA shetani na mbuyu wake, yule straika aliyeachana na Simba kiaina tena baada ya kushindwa kabisa kuisaidia klabu hiyo, Raphael Kiongera ameibukia AFC Leopards ya nchini Kenya tena akiwa moto wa kuotea mbali.


Katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita kati ya Leopards na Thiker United, Kiongera alisaidia upatikanaji wa mabao mawili huku yeye mwenyewe akitupia moja na kuipa ushindi wa mabao 3-0 timu yake mpya kwenye mchezo huo wa mzunguko wa 17 wa ligi kuu ya Kenya KPL.

Kiongera aliyemaliza mkataba wake na Simba alikuwa mwiba mkali katika mchezo huo akiwasumbua walinzi wa kati na wapembeni hali iliyopelekea atajwe katika kikosi cha wachezaji bora wa wiki kwa mujimu Blog bora ya michezo nchini Kenya, Futaa.com


 Echessa kushoto akipambana uwanjaniKatika kikosi hicho cha wiki yumo pia kiungo wa zamani wa Simba, Hillary Echessa ambaye licha ya uveterani wake bado amejihakikishia nafasi ya winga ya kulia katika klabu ya Chemelil Sugar na wikiendi iliyopita aliiua SOFAPAKA kwa bao moja kisha akamtengenezea jingine Laban Gambareko


 Hiki hapa kikosi kamili;
KIKOSI CHA KWANZA:  Ronny Kagunzi, Athman Buki, Ramadhan Yakubu, Charles Momanyi, Shafique Batambuze, Kennedy Muguna, Sunday Mutuku, Robert Omunuk, Hillary Echesa, Bebeto Lwamba, Mungai Kiongera.
 
WACHEZAJI WA AKIBA: Ian Otieno, Luis Masika, Benson Sande, Joash Onyango,  Samwel Olare, Bernard Mang’oli, Meddie Kagere, Kepha Aswani. Moses Mudavadi, John Kago,


 

Post a Comment

 
Top