BOIPLUS SPORTS BLOG

ZURICH, Uswisi

SHIRIKISHO la Mpira wa miguu Duniani FIFA limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaoshindana kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d'Or.

Katika orodha hiyo timu ya Real Madrid imeingiza wachezaji wanne ambao ni Cristiano Ronaldo, Gareth Bale,Toni Kroos na Pepe huku mahasimu wao Barcelona wakiwa na Lionel Messi pamoja na Luis Suarez.

Orodha kamili ya wachezaji hao pamoja na timu wanazochezea:

Gareth Bale ( Real Madrid & Wales)
Gianluigi Buffon (Juventus &Italia)
Antoine Griezmann (Atletico Madrid & Ufaransa)
Toni Kroos (Real Madrid& Ujerumani)
Lionel Messi (Barcelona& Argentina)
Thomas Muller (Bayern Munich & Ujerumani)
Manuel Neuer(Bayern Munich & Ujerumani)
Pepe ( Real Madrid & Ureno)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid & Ureno)
Luis Suarez (Barcelona & Uruguay)

Katika tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kutolewa mwezi Januari mwakani, Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kuinyakua baada ya kuisaidia nchi yake ya Ureno kuchukua kombe la Euro 2016 na klabu ya Real Madrid kubeba kombe klabu bingwa barani Ulaya.

Endapo Ronaldo atanyakua tuzo hiyo atakuwa amechukua mara nne ikiwa ni mara moja nyuma ya mpinzani wake mkubwa Messi ambaye amechukua tuzo hiyo mara tano.

Post a Comment

 
Top