BOIPLUS SPORTS BLOG

SHANGHAI, China
MANCHESTER City imeibuka na ushindi wa penalti 6-5 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye michuano ya Championship iliyoshirikisha timu tatu na kufikia tamati hii leo baada ya sare ya goli 1-1 katika muda wa kawaida.

Mshambuliaji Sergio Aguero aliyetokea benchi kuchukua nafasi Alexandr Zinchenko ndiye aliyefunga goli kwa City dakika ya 64 kabla ya Christian Pulisic kusawazisha kwa penalti dakika 90.

Dortmund ndiyo washindi wa jumla baada ya kupata alama tatu na magoli manne waliyowafunga Manchester United huku City wakiwa na alama 3 baada ya kumalizika kwa mtanange wa Leo.

Mechi kati ya United na City iliahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha na kuufanya uwanja kushindwa kuchezeka hivyo kupelekea miamba hiyo ya jiji la Manchester kusubiri hadi ligi itakapoanza ndiyo wakutane.

Michuano hiyo ilikuwa ikitumiwa na timu hizo ili kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi unakaonza mwezi ujao barani Ulaya.

Post a Comment

 
Top