BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United ipo mbioni kuvunja rekodi ya usajili kwa kumrejesha kiungo wao wa zamani Paul Pogba toka Juventus.

Mabosi wa United walikutana na Juve jana Jumatano ili kumaliza dili huku Mashetani Wekundu wakiwa tayari kulipa pauni 100 milioni na kumfanya Pogba kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.

Kwa sasa rekodi ya mchezaji ghari zaidi duniani inashikiliwa na Gareth Bale aliyesajiliwa na Real Madrid akitokea Tottenham Hotspur kwa pauni 85 milioni mwaka 2014.


Pogba aliwahi kuwatumikia Mashetani hao kwa miaka mitatu kabla ya mwaka 2012 kutimkia Juve baada ya kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya Sir Alex Ferguson.

Endapo United watafanikiwa kunasa saini ya mfaransa huyo utakuwa ni usajili wa nne baada ya Erick Baily,Zlatan Ibrahimovic na Henrick Mikhtarian uliofanywa na kocha mpya Jose Mourinho.

Post a Comment

 
Top