BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
KOCHA wa timu ya Medeama FC toka Ghana Prince Yaw Owusu amekiri mchezo wao wa kesho kombe la shirikidho barani Afrika dhidi ya Yanga utakuwa mgumu kutokana na wapinzani hao kupoteza michezo miwili huku wakicheza katika ardhi ya nyumbani.

Mtanange huo utachezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam saa 10 jioni huku wageni hao wanatarajiwa kuingia uwanjani kwa tahadhari kubwa kutoka na wapinzani wao kujeruhiwa mara mbili.

Kocha huyo alizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika katika uwanja wa taifa ambapo alisema watajitahidi kutafuta goli la mapema ili warudi nyuma kuwazuia Yanga wasipate goli.

"Tutacheza kwa tahadhari kubwa, wenzetu wapo nyumbani wana faida kutoka kwa mashabiki lakini sisi tutatafuta goli la mapema ili turudi nyuma kuzuia," alisema kocha Owusu.


Madeama wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama moja katika msimamo wa kundi A baada ya kufungwa mchezo wa kwanza dhidi ya TP Mazembe na kutoka sare na Mo Bejaia.

Endapo Yanga itashinda mchezo huo itapanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu na ikipoteza itakuwa na nafasi finyu ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali.

Post a Comment

 
Top