BOIPLUS SPORTS BLOG

Sheila Ally, Dar

KOCHA wa zamani wa Mbeya City na Ndanda FC,  Meja mstaafu Abdul Mingange huenda akasaini mkataba wa kuifundisha Prisons akichukuwa nafasi ya Salum Mayanga ambaye amerudi kuifundisha Mtibwa Sugar.

Msimu uliopita Mingange amefundisha timu mbili alianza na Mbeya City ambapo ilipata matokeo mabaya yaliyotishia timu hiyo kushuka daraja na kuamua kuachana naye ambapo walimleta Mmalawi, Kinnah Phiri.

Baadaye Mingange alikwenda Ndanda FC ya mjini Mtwara ambako pia hakupata bahati kwani timu yake haikufanya vizuri hivyo uongozi wa Ndanda kuamua kumchukuwa Hamsin Malale kutoka JKU ya Zanzibar. Phiri na Malale waliweza kuzinusuru timu hizo kushuka daraja.

Habari kutoka ndani ya Maafande hao, zinasema kwamba viongozi wa Prisons walikuwa na kikao cha mwisho na kocha huyo ambapo mazungumzo yao yamefikia pazuri huku Katibu Mkuu wa Prisons, Osward Morris akithibitisha hilo.

"Ni kweli tumefanya mazungumzo naye ila bado hatujampa mkataba, nadhani mpaka kesho Jumanne tutakuwa tumeweka mambo sawa, ila ni kocha ambayo yupo kwenye mipango yetu," alisema Morris.

Post a Comment

 
Top