BOIPLUS SPORTS BLOG

BARCELONA, Hispania

MCHEZAJI bora wa dunia mara tano raia wa  Argentina  Lionel Messi amehukumiwa kifungo cha miezi 21 jela baada ya kupatikana na makosa ya kutumia ulaghai wakati wa ulipaji ushuru.

Vyombo vya habari nchini Uhispania vimeripoti hukumu hiyo huku staa huyo Barcelona akionekana alifanya kosa hilo kwa kukusudia.

Babake, Jorge Messi, pia amehukumiwa kufungwa jela kwa kuilaghai Uhispania dola 4.1milioni  kati ya 2007 na 2009.

Wakati wa kesi hiyo waendesha mashtaka walisema maeneo salama yenye kinga dhidi ya ushuru ni Belize na Uruguay ambayo ndiyo yalitumiwa kuficha mapato kutokana na uuzaji wa haki za picha za mchezaji huyo.

Lakini Messi amesema hakufahamu lolote kuhusu masuala yake ya kifedha huku akitarajiwa kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.

Post a Comment

 
Top