BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
Ibrahim Twaha 'Messi' akisaini kandarasi ya kuichezea Kagera Sugar

TIMU ya Kagera Sugar imepania kufanya vizuri katika msimu ujao baada ya kuendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wawili wazoefu na mikikimikiki ya ligi kuu Tanzania bara.

Wachezaji hao ni golikipa Hussein Sharif 'Cassilas' na winga Ibrahim Twaha 'Messi' kwa ajili ya kuongeza kasi kwa Wanankulumbi hao ambao msimu uliopita hawakuwa katika ubora mzuri.

Kocha mpya wa timu hiyo Mecky Mexime ameiambia BOIPLUS kuwa anaendelea kuimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wazuri ambao wataziba mapengo kulingana na mapungufu yaliyojitokeza msimu uliopita.

"Ni kweli tunewasajili Cassilas na Messi kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya kikosi, tunaamini kutokana na uzoefu wao wa ligi watakuwa msaada mkubwa kwetu," alisema Mexime.


Cassilas 'akianguka' jana tayari kwenda kulilinda lango la Kagera

Msimu uliopita kocha huyo pamoja na Cassilas walikuwa wakiwatumikia wakata miwa wa Mtibwa Sugar huku Messi akiwa na Wagosi wa kaya Costal Union ambao wameshuka daraja na kuweka nia ya dhati ya kurejesha makali yaliyopotea katika siku za karibuni.

Nahodha huyo wa zamani wa Mtibwa na timu ya taifa alijiunga na wakata miwa hao mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kutimuliwa Adolf Rishard aliyeweza kuinusuru na janga la kushuka daraja.

Kagera ni miongoni mwa timu zinazotoa upinzani wa kweli katika ligi kuu kwa misimu kadhaa iliyopita licha ya mwaka jana kupita katika wakati mgumu.

Post a Comment

 
Top