BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
KIUNGO mkabaji wa wekundu wa Msimbazi Simba, Jonas Mkude ametua nchini juzi akitokea Afrika ya Kusini alikoenda kufanya majaribio na kwamba sasa yuko tayari kwenda kujiunga na wenzake mjini Morogoro.

Akizungumza na BOIPLUS akiwa nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo, kiungo huyo kipenzi cha wanasimba alisema yupo hapa kwa siku tatu kwa ajili ya mapumziko kabla hajajiunga na timu.

"Nilikuwa mapumzikoni tu baada ya kutoka Sauzi, ila sasa niko fit kabisa kuanza mazoezi na kesho naenda kambini Moro," alisema Jonas.

Akizungumzia taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa alipata ajali ya gari jana usiku maeneo ya Kimara, Mkude alisema "Hata sielewi kwanini hawa watu wanapenda kunichafua, mimi niko nyumbani na sijapata ajali yoyote. Naona sasa umekuwa mtindo watu kunizushia habari za kuniharibia, hii ni lazima nitaichukulia hatua, siwezi kuendelea kukaa kimya."

Simba wameweka kambi mjini Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu msimu ujao ambapo wachezaji kadhaa wa kigeni wanafanyiwa majaribio. Tayari Simba imempoteza kiungo Justice Majabvi huku pia ikifahamika kuwa kama Mkude atafuzu majaribio yake huko Afrika Kusini basi watalazimika kupata watu mahiri wa kuziba nafasi hizo.

Post a Comment

 
Top