BOIPLUS SPORTS BLOG

SHANGHAI, China
MANCHESTER United imekubali kichapo cha magoli 4-1 toka Borussia Dortmund katika michuano ya Championship inayoshirikisha timu tatu huko nchini China.

Michuano hiyo inashirikisha timu za United, Dortmund pamoja na Man City ikiwa ni kuziandaa timu hizo kabla ya kuanza kwa mikikimikiki ya ligi mbali mbali barani Ulaya.

Vijana wa kocha Jose Mourinho walionekana kuzidiwa ujanja tangu mwanzoni mwa mchezo ambapo dakika ya 19 Gonzalo Castro aliipatia Dortmund goli la kwanza baada ya kupiga mpira uliomshinda golikipa Johnstone.

Magoli mengine yalifungwa na Pierre Aubemeyang kwa mkwaju wa penalti, Ousmane Dembele na Castro alimalizia la nne huku lile la United likifungwa na Henrick Mikhtarian baada ya kazi nzuri ya Juan Mata.

Huu ni mchezo wa pili wa kocha Mourinho tangu alipoanza kukinoa kikosi hicho baada ya ule wa awali kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Wigan Athletic.

Post a Comment

 
Top