BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester United imethibitisha kumsajili kiungo mshambuliaji raia wa  Armenia anayekipiga Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan.

Kiungo huyo mwenye miaka 27 amesaini mkataba wa miaka minne ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi na kuigharimu United pauni 26.3 milioni.

Mikhitaryan alisema: "Nina furaha kujiunga na  Manchester United. Ndoto zangu zimekuwa kweli. 
Najisikia fahari kucheza klabu kubwa kama hii yenye historia ya kupendeza. Namshukuru  Jose Mourinho kwa kuniamini na kunijumuisha katika kikosi chake."


"Mwisho, Nina amini kucheza katika klabu hii itakuwa ni kumbukumbu nzuri kwa baba yangu kwa kunihamasisha hadi kufikia hapa nilipo leo."

Kwa upande wake Kocha Mourinho alisema "Henrikh ni mchezaji mwenye kipaji na amekuwa na mafanikio kuanzia kwenye nchi yake hadi klabu.

" Anaweza kucheza kitimu, ana ujuzi na ana muono mzuri mbele goli.Ninayo furaha kumtangaza kuwa mchezaji wa  United."

Mkhitaryan ameifungia Dortmund magoli  23 kwenye ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga katika miaka mitatu aliyodumu na klabu hiyo.

Post a Comment

 
Top