BOIPLUS SPORTS BLOG

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA mpya wa klabu ya ​ Manchester United  Jose Mourinho amewataka mashabiki wa timu hiyo kumuunga mkono baada ya miaka miwili migumu chini ya meneja Louis van Gaal na kukosa imani nae hadi kufikia hatua ya kumzomea kwa kushindwa kufanya vizuri.

Mreno huyo alisema kuwa ana matarajio makubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kushangilia timu yao huku akitanabaisha kuwa wana mapenzi makubwa na timu yao.

"Najua wana matarajio makubwa kutoka kwangu na mimi pia vivyo hivyo, hatutakuwa na nafasi ya kuwa na furaha kama hatutakuwa pamoja ila nina amini wana mapenzi makubwa na timu yao.

"Ni ukurasa mpya katika maisha ya klabu, unapobadili kocha kunakuwa ni kipindi cha huzuni, tutaongeza nguvu ndani ya kikosi na kubaki na wachezaji waliopo ili tuwe na timu ya ushindani msimu ujao.

"Furaha ya mashabiki ni timu kufanya vizuri nami nipo kwa ajili hiyo. Nilipofika nilikabidhiwa jezi ya United, ninaipenda na pia nina furaha kuiwakilisha, nitafanya kila linalowezekana kuwafanya watu wawe na furaha," alisema Mourinho.

 Kocha huyo mwenye maneno mengi alisema kuwa anategemea makubwa kutoka kwa wachezaji wake aliowasajili kushirikiana waliopo kutengeneza kikosi imara.

" Nahitaji kushinda kila mchezo, kucheza soka safi, kufunga magoli mengi na kutoruhusu kufungwa japokuwa wapinzani nao wanajipanga," alisema Mourinho.

Post a Comment

 
Top