BOIPLUS SPORTS BLOG

SHANGHAI, China
MECHI kati ​ ya Manchester united na City iliyokuwa ichezwe leo Jumatatu katika michuano ya Championship inayofanyika nchini China imeahirishwa kutokana na hali mbaya ya hewa iliyosabibisha uwanja usichezeke. 

Hii ni mechi ambayo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa ikiwakutanisha miamba hiyo ya jiji la  Manchester kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza itakayoanza Agosti 14.

Mvua kubwa iliyonyesha siku chache zilizopita imepelekea kulowesha sehemu ya kuchezea ambayo ingeweza kusababisha majeruhi kwa wachezaji endapo wangecheza katika hali hiyo.

Mchezo huo ulikuwa uwakutanishe makocha mahasimu Jose Mourinho wa United na Pep Guardiola anayekinoa kikosi cha City ambao wamekuwa na ushindani mkubwa wanapokutana tangu walipokuwa nchini Hispania.

Katika mchezo wa awali United ilikubali kichapo kikali cha magoli 4-1 toka kwa Borussia Dortmund na kuwaacha vijana wa Mourinho wakibaki midomo wazi.

Michuano hiyo pia hutumiwa kuandaa vikosi kuelekea kufungua pazia za ligi mbali mbali barani Ulaya zitakazoanza mwezi ujao na inashirikisha timu tatu ambazo ni United, City na Dortmund.

Post a Comment

 
Top