BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar

WACHEZAJI wa timu Yanga wametakiwa kujiamini na kujituma katika mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Medeama ili kuibuka na ushindi.

Wapinzani hao toka nchini Ghana tayari wameshaingia jijini Dar es Salaam na leo watafanya mazoezi katika uwanja wa taifa tayari kwa mchezo huo kesho jioni.

Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi ameiambia BOIPLUS kuwa wamewasisitizia wachezaji wao kutumia nafasi zinazopatikana kwakuwa huo ndio ugonjwa mkubwa unaowasumbua.

"Tunatengeneza nafasi nyingi lakini hatuzitumii, wenzetu wanapata chache na wanatuadhibu. Tunahitaji wachezaji wetu wajiamini na watumie nafasi ili tushinde mchezo," alisema Mwambusi.

Yanga jana walikuwa wakifanya mazoezi katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam huku mshambuliaji Amissi Tambwe akirejea dimbani baada ya kupona Malaria.

Yanga wanatakiwa wafanye kila linalowezekana kuibuka na ushindi katika mtanange huo baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Mo Bejaia ugenini na TP Mazembe nyumbani.

Post a Comment

 
Top