BOIPLUS SPORTS BLOG

Akram Msangi, Dar

UONGOZI wa klabu ya Simba umeingia kandarasi ya miaka miwili na kocha Joseph Omog raia wa Cameroon kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kuanzia msimu ujao.

Kandarasi hiyo ilifanyika mbele ya waandishi wa Habari katika hotel ya Regency Peacock ambapo Omog amewaahidi Wanasimba kurejesha heshima iliyopotea kwa miaka kadhaa sasa.


"Nachukua nafasi hii kuwatambulisha kocha wetu mpya ambaye tumesaini nae mkataba nanyi mkishuhudia. Nawaomba Wanasimba wote nchi nzima kumpa ushirikiano wa kutosha kwa ajili yetu sote," alisema Aveva.

Pia katika mkutano huo na waandishi wa Habari Aveva alimtambulisha Katibu mkuu mpya wa klabu hiyo Patrick Kahemele ambaye aliteuliwa siku za karibuni kwa ajili ya kuratibu shughuli zote za Wekundu hao.


"Napenda kuchukua nafasi hii pia kuwatambulisha katibu wetu mkuu ndugu Kahemele ambaye atakuwa hapa kwa ajili ya kuratibu shughuli zote za klabu kuanzia leo," alisema Aveva.


Omog anachukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Dylan Kerr ambayo baadae ilikaimiwa na Mganda Jackson Mayanja.

Post a Comment

 
Top