BOIPLUS SPORTS BLOG

PRETORIA, Afrika Kusini

BINGWA wa mbio za Olimpiki kwa walemavu Oscar Pistorius, raia wa Afrika Kusini, amehukumiwa kufungwa jela miaka sita kwa kosa la kumuua mpenzi wake mwaka 2013.

Pistorius mwenye umri wa miaka 29 
alimpia risasi mara nne za kifua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari 14, 2013.

Pistorius alikuwa akikabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela zaidi ya miaka 15.

Mawakili wa upande wa mashtaka na wa upande wa mshtakiwa wanaweza kukata rufaa.

Uamuzi huo wa mahakama nchini Afrika Kusini umetolewa baada ya kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia ikiyotolewa  mwezi Desemba mwaka jana.

Mshitakiwa amepelekwa jela ya Khosi Mampuru mjini Pretoria.

Post a Comment

 
Top