BOIPLUS SPORTS BLOG

PARIS, Ufaransa

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameuonyesha umma kuwa yeye ni mtu wa ajabu baada ya kuamua kumkabidhi kiungo Luis Nani kiatu cha Silva alichopewa kama zawadi baada ya kufunga mabao matatu na kusaidia upatikanaji wa mengine mawili kwenye Michuano ya EURO 2016.

Kiatu cha dhahabu katika michuano hiyo iliyomalizika jana kwa Ureno kuibuka mabingwa kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ufaransa, kilinyakuliwa na Antoine Griezmann aliyefanikiwa kufunga mabao sita na kusaidia upatikanaji wa mengine mawili.

Baada ya kukabidhiwa kiatu hicho,  Nani aliyechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa ubingwa huo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram maneno ya kumshukuru Ronaldo huku akimtaja kuwa zaidi ya nahodha na ni bingwa wa ukweli.


Post a Comment

 
Top