BOIPLUS SPORTS BLOG

GENK, Ubelgiji

STRAIKA mtanzania Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, usiku wa leo amecheza mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano ya EUROPA na kuisaidia timu yake kuibuka na udhindi wa mabao 2-0 dhidi ya Budućnost ya Montenegro.

Genk walioanzia hatua ya mtoano ya michuano hiyo walipata bao la kwanza kwa njia ya penati kupitia kwa Neeskens Kebano katika dakika ya 27, bao ambalo liliwapeleka mapumziko.

Vijana wa Peter Maes waliingia kipindi cha pindi kama nyuki waliochokozwa huku wakionyesha wazi wana nia ya kupata ushindi mnono nyumbani, walipata bao la pili katika dakika ya 79 likiwekwa nyavuni na Samatta kufuatia kazi nzuri ya winga wa Jamaica, Leon Bailey.

Kwa ushindi huo sasa Genk wanahitaji kupata japo sare tu katika mchezo wa marudiano ili wasonge. Mchezo wa pili utachezwa nchini Montenegro Julai 21.

Post a Comment

 
Top