BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
MSAFARA wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, uliondoka jana alfaji umefika  salama jijini Antananarivo, Madagascar kwa ajili kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6.

Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21 katika Uwanja wa Azam, ulioko Chamazi Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na kwamba mshindi atakuwa amejiwekea mazingira mazuri ya kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana, zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.

Mkuu wa msafara ni Ayoub  Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana, maofisa wengine waliosafiri na timu hiyo ni Kocha Mkuu Bakari Shime, Daktari wa timu Shecky Francis Mngazija na Mtunza Vifaa, Andrew Vanance Andrew.

Pia yumo Juma Kaseja  ambaye kwa muda amechukua nafasi ya makocha wasaidizi, Sebastian Nkoma na Muharam Mohammed ‘Shilton’ wanaohudhuria kozi ya makocha ngazi ya juu inayoratibiwa na CAF.

Nyota waliosafiri ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda, Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.

Viungo ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma, Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar Mkomola na Muhsin Malima Makame.

Post a Comment

 
Top