BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
Mayenge Bionik kushoto alipowasili uwanja wa ndege pamoja na Masanga Masudi Cedrick , wachezaji hao walipokelewa na Katibu mkuu wa Simba, Patrick Kahemele

NI kama imepania kurejea katika ubora wake baada ya misimu minne, timu ya  Simba imeshusha 'injini' mbili toka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ajili ya kufanya majaribio kabla ya kujiunga na Wekundu hao.

Wachezaji hao ni kiungo ambaye anaweza kucheza namba nyingi uwanjani Masanga Masudi Cedric anayekipiga Sanga Balende ya DR Congo na mwingine ni beki Mayenge Bionik anayechezea FC Lupopo.

Katibu mkuu wa Simba Patrick Kahemele ndiye aliyewapokea wachezaji hao katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jana ambapo  wataungana na wenzao wanaojifua vikali mkoani Morogoro mchana wa leo.

Kahemele ameiambia BOIPLUS kuwa  "Tumewapokea wachezaji wawili raia wa Kongo wamekuja kufanya majaribio na leo wataungana na wenzao mkoani Morogoro, endapo watafaulu watasajiliwa moja kwa moja," alisema Kahemele.

Mtandao huu jana uliongea na Makamu wa Rais wa klabu hiyo Godfrey Nyange 'Kaburu' na kutanabaisha kuwa bado wanaendelea kupokea wachezaji wa kigeni wanaokuja kufanya majaribio ili kuangalia uwezekano wa kuwasajili.

Wachezaji hao wataungana na wakongomani wenzao Moussa Ndusha na Janvier Bukungu pamoja na mshambuliaji Blangnon Fedrick raia wa Ivory Coast bila kumsahau beki Method Mwanjala toka Zimbabwe.

Post a Comment

 
Top