BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu
KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Tanzania 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa ameahirisha kambi ya timu hiyo iliyokuwa ianze Agosti mosi kutokana na maombi ya klabu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutaka kujiandaa vizuri na msimu mpya wa ligi.

Wachezaji ambao Mkwasa amewaita wanatoka kwenye klabu mbalimbali na ambazo zinaongoza kutoa nyota wengi ni Simba, Yanga, Azam pamoja  na Mtibwa Sugar FC.

Hivyo basi, Mkwasa sasa atakuwa anafuatilia mwenendo wa nyota 24 aliowaita kwenye michezo mbalimbali ya kirafiki ya klabu hizo inayofanyika kabla ya kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara na michezo ya raundi ya kwanza na pili ya Ligi Kuu kabla ya kukiita tena kikosi hicho kwa ajili ya safari ya kwenda Nigeria.

Taifa Stars ina mchezo dhidi ya Nigeria utakochezwa jijini Lagos, Septemba 2, 2016 ambao ni wa kukamilisha ratiba katika kundi G baada ya Misri kusonga mbele wakati Chad kujitoa.

Post a Comment

 
Top