BOIPLUS SPORTS BLOG

ZURICH, Uswisi

SHIRIKISHO la kandanda duniani FIFA limetoa viwango vya ubora wa nchi wanachama wake kwa mwezi Juni huku ikishuhudiwa Tanzania ikipaa kwa nafasi 13 kuelekea juu.

Tanzania iliyokuwa katika nafasi ya 136 , imefanikiwa kukwea mpaka nafasi ya 123 lakini ikashindwa kuwapiku majirani zake  Kenya waliotisha kwa kupanda kwa nafasi 43 na kuipeleka hadi nafasi ya 86 katika viwango hivyo. 

Ureno ambao ni mabingwa wapya wa Euro 2016 wao wamepanda mpaka nafasi ya 6 wakati Chile ambao ni mabingwa wa Copa America wanakamata nafasi ya tano huku Argentina wakiendelea kukamata uongozi kwa kukamata nafasi ya kwanza katika chati hiyo ikifuatiwa na Ubelgiji.

Kwa upande wa Afrika Algeria imeendelea kushika usukani kwa kuwa ya kwanza katika bara la Afrika huku ikishika nafasi ya 32 katika ubora.

Kumi Bora Barani Afrika
Algeria (32)
Ivory Coast (35)
Ghana (36)
Senegal (41)
Misri (43)
Tunisia (45)
Cameroon (53)
Morocco (54)
DR Congo(59)
Mali (61)

Kumi Bora Duniani
Argentina
Ubeljiji
Colombia
Ujerumani
Chile
Ureno
Ufaransa
Spain
Brazil
Italia

Post a Comment

 
Top