BOIPLUS SPORTS BLOG

Mpiga Picha Wetu, Morogoro
SIMBA wame'miss' raha kwa muda mrefu sana, lakini kuna kila dalili kuwa Wekundu hao wameamua kuachana na maisha ya unyonge kwa kufanya usajili wa kimya kimya ila unaoonyesha kutimiza mahitaji ya timu.

 Huyu hapa ni straika mpya Blagnon Goue Fredric kutoka nchini Ivory Coast. Hapa ndipo yalipolala matumaini ya vigogo hao kutoka mtaa wa Msimbazi.

 Matumaini yote hayo yatawezeshwa na 'Wanaume' wawili wa shoka, Kocha Mkuu Joseph Omog (kulia) na msaidizi wake Jackson Mayanja. Hapa walikuwa wakipanga mikakati yako katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom.

Blagnon aaliyekuwa akiichezea African Sports ya nchini kwao, aliletwa na kipa Vicent Angban huku akiwahakikishia wekundu hao kuwa wasahau kuhusu ukame wa mabao.

Matumaini haya yataendana na matokeo?, ni suala la muda tu. 

Post a Comment

 
Top