BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi Wetu
WANACHAMA wa Simba tawi la SDF lenye makao makuu yake Tabata Kimanga, leo wameikaribisha wiki ya Simba kiaina yake kwa kwenda kufanya usafi katika Zahanati ya Tabata huku pia wakitoa msaada wa vifaa.

Akizungumza na BOIPLUS mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Afisa habari wa SDF, Ally Shatry 'Bab Chicharito'  alisema waliamua kufanya jambo hilo kwa sababu kuu tatu."Kwanza ni katika kutimiza wajibu wetu kwa jamii, pili ni kutimiza agizo la Rais John Magufuli kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku maalumu ya usafi lakini tatu ni kuikaribisha wiki ya Simba inayoanza rasmi kesho," alifafanua Bab Chicharito.

Misaada iliyotolewa na wanachama hao ni pamoja na sabuni ya unga na vipande, dawa za kuulia wadudu, fagio, maji ya kunywa, mikate na vifaa vingine vya kufanyia usafi.


Mwenyekiti wa tawi la SDF, Karim Boimanda akikabidhi msaada wa tawi hilo kwa muuguzi mkuu wa Zahanati hiyo

Kwa upande wake Dr Mtei aliyemwakilisha Mganga Mfawidhi alisema "nimeshangazwa sana na hiki kilichotokea, sijawahi kuona mtu yeyote au kikundi kikija hapa na kufanya haya mliyoyafanya, ahsanteni sana. Naamini wengine wakiona wataiga mfano huo."

SDF ni tawi la Simba lililozinduliwa na rasmi na Rais wa klabu hiyo Evance Aveva mwezi Oktoba mwaka jana lakini limekuwa moja ya matawi maarufu nchini kutokana na utaratibu wake wa kipekee katika uendeshaji.


Wanachama wa SDF wakigawana vifaa vya kufanyia usafi kabla ya kuanza zoezi hilo

Wauguzi wa Zahanati hiyo nao hawakubaki nyuma, kulia ni mama mkunga akimwelekeza jambo mwanachama wa SDF, Khalid Mwichande

Mjumbe wa Kamati ya Sherehe na Maafa ya SDF, Magesa Mkome akiwajibika 

Mhasibu wa SDF, Bernard Chezue akijiandaa kuanza kufanya usafiKatibu wa Kamati ya Sherehe na Maafa ya SDF, Mohamed Nammenge akiondoa takataka zilizojificha kwenye majaniMwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Uchumi ya SDF, Mathew Kawogo 'Kiongozi' kulia akishirikiana na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya SDF, Hamza Mahosanya kusafisha lango la kuingilia maabara

Baada ya kazi, wekundu hao wa SDF walibadilishana mawazo kabla hawajarejea tawini

Post a Comment

 
Top