BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar 
TIMU ya Temeke Market imetangazwa kuwa mabingwa wapya wa Sports Xtra Ndondo Cup baada ya kuifunga Kauzu FC magoli 3-1 katika uwanja wa Bandari jijini Dar es Salaam.

Hii ni fainali ya pili kwa Kauzu  kupoteza baada ya mwaka jana pia kupoteza mbele ya Faru Jeuri na kuonekana kutokuwa na bahati na michuano hiyo.

Waziri wa Habari,Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi akiambatana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwaongoza mamia ya wakazi wa jiji kushuhudia fainali hiyo. 

Magoli ya Temeke yaliwekwa kimiani na Ramadhani Madebe, Shaban Kisiga na Adam Kingwande huku lile la kufutia machozi la Kauzu likifungwa na Rashidi Gumbo.

Mabingwa wapya Temeke Market wamejinyakulia kitita cha sh 10 milioni huku washindi wa pili Faru Jeuri wakipata sh 5 milioni.

Kiungo mkongwe Shabani Kisiga 'Malone' ndiye mchezaji bora wa Fainaili akizawadiwa kiasi cha sh 50,000 na pia kuibuka mchezaji bora wa michuano na kunyakua kitita cha shilingi 1 milioni.

Post a Comment

 
Top