BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepania kutoa kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi.

Hapo awali madawati ya wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea au wa muda na sasa shirikisho hilo linataka kuajiri wafanyakazi.

Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwake  ikiwa ni uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaa za soka la wanawake.

Kuhusu waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi na viwango vya Kimataifa.

Wakati huohuo, TFF inatarajia kuimarisha Kurugenzi yake ya masoko ambako sasa ataajiriwa Mkurugenzi wa masoko na habari.
Lengo hasa ni kuendana na hali halisi ya uendeshaji mpira duniani ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa soka.

"Lengo ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpira wa miguu zinatokana na mpira  na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati muafaka" alisema Mwesigwa Selestine.

Post a Comment

 
Top