BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

TIMU ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni ya Tanzania imepangwa kucheza na Ivory Coast kati ya Agosti 26, 27 au 28, kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017 zitakazofanyika Lagos, Nigeria. 

Fainali za Mpira wa Miguu Ufukweni ambazo zitafahamika pia kama 2016 CAF Beach Soccer Championship, zitafanyika kuanzia Desemba 13 hadi 18,  jijini Lagos, Nigeria kwa kushirikisha timu nane.

Tayari Nigeria imepasishwa kuwa mshiriki kwa sifa ya uenyeji wakati timu nyingine 14 zinawania kucheza fainali hizo. 

Timu nyingine zinazowania ni:

Cape Verde v Senegal

Uganda v Misri

Liberia v Morocco

Kenya v Ghana

Msumbiji v Madagascar

Sudan v Libya.

Post a Comment

 
Top