BOIPLUS SPORTS BLOG

LUBUMBASHI, DRCongo
TIMU ya TP Mazembe imejihakikisha kutinga hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga Mo Bejaia goli 1-0 katika uwanja wa Mazembe Arena.

Mchezo huo wa jioni ya leo ulikuwa wenye kasi kubwa huku wenyeji wakionekana kuhitaji matokeo ya ushindi ili kujihakikisha nafasi ya kutinga nusu fainali.

Mshambuliaji Rainford Kalaba raia wa Zambia ndiye aliyeifungia Mazembe goli hilo pekee dakika ya 61 baada ya umakini hafifu wa mabeki wa Bejaia.

Matokeo hayo yamewafanya Mazembe kujikita kileleni mwa kundi hilo baada ya kujikusanyia alama 10 wakifuatiwa na Bejaia huku Medeama wakikamata nafasi ya tatu na Yanga wakiburuza mkia.

Katika kundi hilo kila timu imebakiwa na mechi mbili mkononi huku timu za Medeama na Bejaia zikichuana vikali ili kuambatana na Mazembe kufuzu katika hatua ya nusu fainali.

Post a Comment

 
Top