BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania TFF limewatangazia wanamichezo wote  kuwa  hafla ya ugawaji tuzo za washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2015/2016 itafanyika Jumapili Julai 17 katika hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam.

Aina 13 za tuzo za Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa kwa washindi chini ya uratibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi  na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).

Tuzo hizo na kiasi cha fedha wanazopata washindi kwenye mabano ni

Bingwa (sh. 81,345,723
Makamu bingwa (sh. 40,672,861)
3. Mshindi wa tatu (sh. 29,052,044)
4. Mshindi wa nne (sh. 23,241,635)
5. Timu yenye Nidhamu Bora (sh17,228,820)

Zilizopendekezwa kuwania tuzo hiyo ni:
- JKT Ruvu
- Mgambo Shooting na
- Mtibwa Sugar

6. Mchezaji Bora wa Ligi (sh. 9,228,820)

Waliopendekezwa ni kuwania tuzo hiyo ni:
- Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar)
- Juma Abdul (Yanga) na
- Mohamed Hussein (Simba)

7. Mfungaji bora (sh. 5,742,940)
8. Kipa Bora (sh. 5,742,940)
Waliopendekezwa  kuwania tuzo hiyo ni:
- Aishi Manula (Azam),
- Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na
- Deogratius Munishi (Yanga)

9. Mchezaji Bora wa Kigeni (sh. 5,742,940)
- Donald Ngoma (Yanga)
- Thabani Kamusoko (Yanga)
- Vincent Agban (Simba)

10. Kocha Bora (sh. 8,000,000)
Waliopendekezwa  kuwania tuzo hiyo ni:
- Hans Van Pluijm (Yanga)
- Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na
- Salum Mayanga (Tanzania Prisons)

11. Mwamuzi bora (sh. 5,742,940)
Waliopendekezwa  kuwania tuzo hiyo ni:
- Anthony Kayombo
- Ngole Mwangole
- Rajab Mrope

12. Mchezaji Bora Chipukizi (sh. 4,000,000
Waliopendekezwa  kuwania tuzo hiyo ni:
- Farid Mussa (Azam)
- Mohamed Hussein (Simba)
- Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na
- Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar)

13. Goli bora la msimu (sh. 3,000,000)
Kinyang'anyiro cha goli bora ni:
- Ibrahim Ajib (magoli mawili ) na
- Amisi Tambwe (goli moja)

Post a Comment

 
Top