BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
MSHAMBULIAJI wa TP Mazembe ya DR Congo, mtanzania Thomas Ulimwengu huenda akaukosa mchezo wa marudiano wa timu yake dhidi ya Mo Bejaia ya nchini Algeria kutokana na majeraha. Mchezo huo utapigwa jijini Lubumbashi katikati  wa wiki ijayo.

Akizungumza na BOIPLUS kutoka Lubumbashi, Ulimwengu alisema ameumia Ligamenti baada ya kufanyiwa madhambi leo katika mchezo wa kirafiki kati ya timu yake na KAF ambayo ni ya Lubumbashi pia.


"Ninahisi maumivu makali sana, kesho nitarudi hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi baada ya hapo ndio nitajua nitakaa nje kwa muda gani," alisema Ulimwengu.

Mazembe inacheza mechi za kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Bejaia ambapo Ulimwengu amekiri haoni uwezekano wa yeye kucheza mechi hiyo kutokana na maumivu anayoyasikia.Katika kundi A Mazembe wanaongoza wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na Bejaia wenye pointi tano. Medeama wana pointi mbili na Julai 27  wanawakaribisha Yanga wanaoburuza mkia wakiwa na pointi yao moja.

Post a Comment

 
Top