BOIPLUS SPORTS BLOG

Mwandishi wetu

WAPINZANI  wa Yanga katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika, timu ya  Medeama kutoka Ghana, itawasili jijini Dar es Salaam keshokutwa Alhamisi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ).

Yanga itaikaribisha Medeama ikiwa ni mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi mchezo utafanyika saa 10.00 jioni katika  Uwanja wa Taifa, Jumamosi Julai 16.

Huu ni mchezo wa tatu kwa Yanga katika harakati za kuwania Kombe la shirikisho hatua ya makundi. Michezo miwili ya awali ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa hapa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour.

Kamishna wa mchezo huo atakuwa Pasipononga Liwewe kutoka Zambia na maofisa wasimamizi ni Mfubusa Bernard ambaye atasimamia utendaji wa waamuzi wakati Mratibu Mkuu wa mchezo huo kutoka CAF atakuwa Ian Peter Keith Mc Leod.

Post a Comment

 
Top