BOIPLUS SPORTS BLOG

LONDON, Uingereza

KLABU ya Arsenal imeripotiwa kuandaa kitita cha pauni 34 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Olympic Lyon  Alexandre Lacazette.

Washika bunduki hao wako tayari kupeleka ofa kwa Lyon baada ya kumkosa Jamie Vardy wa Leicester City aliyekuwa akipatikana kwa dau la pauni 20 milioni.

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekuwa akivutiwa na mshambuliaji huyo mwenye miaka  25 ili kuongeza chachu katika safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Oliver Giroud. 

Wagonga nyundo wa jiji la London West Ham United pia wako katika mbio za kumuwinda mshambuliaji huyo ambapo taarifa zinasema Maofisa wa klabu hiyo walisafiri hadi Lyon kwa ajili ya kufanya makubaliano lakini dili  likakataliwa.

Juhudi za kumbakisha mshambuliaji huyo zinasaidiwa na timu hiyo kushiriki michuano ya ligi mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Post a Comment

 
Top