BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar
KILE kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu na wanachama wa Simba kimetimia baada ya mkutano mkuu kuridhia mabadiliko ya katiba ili kuingia katika mfumo wa Hisa.

Wajumbe wa mkutano huo ambao ulikuwa na ajenda 10 walionyesha tangu mwanzo kutaka mabadiliko huku wakiisubiri kwa hamu ajenda ya tisa ambayo ndiyo imekamilika kwa wanachama kupitisha mapendekezo hayo kwa kauli moja.

Baada ya ajenda hiyo Rais Evance Aveva alifunga mkutano huo na kuwaacha wanachama wakishangilia kwa nguvu.

Kutokana na ridhaa hii ya wanachama, Simba italazimika kuandaa mchakato wa jinsi gani sahihi ya kuingia katika mfumo wa Hisa huku Mfanyabiashara Mohamed Dewji 'Mo' akipewa nafasi kubwa zaidi ya kuwa mwekezaji mkuu.

Post a Comment

 
Top