BOIPLUS SPORTS BLOG

Zainabu Rajabu, Dar
KUTOKANA na kucheza mechi nyingi bila kumpumzika mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga imeonyesha hofu ya kuboronga mechi zake za mwanzoni mwa ligi kuu ya Vodacom.

Tangu kumalizika kwa ligi msimu uliopita mabingwa hao hawajawahi kupumzika kutokana na kushiriki klabu bingwa barani Afrika kabla ya kutolewa na kucheza kombe la shirikisho ambapo wanaendelea na mechi za hatua ya makundi.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Juma Mwambusi ameiambia BOIPLUS kuwa msimu utakaoanza mwezi ujao utakuwa mgumu kwao kutokana na wachezaji wake kucheza mechi nyingi za ndani na nje bila kupata muda wa kupumzika.

"Tutakuwa katika wakati mgumu msimu ujao kutokana uchovu wa wachezaji wetu, lakini bado hatukati tamaa ya kutetea ubingwa wetu," alisema Mwambusi.

Yanga inaendelea kushiriki michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika ambapo mpaka sasa wamejikusanyia alama moja pekee katika kundi A huku wakiburuza mkia.

Agosti 14 mabingwa hao watateremka dimbani kumenyanya na MO Bejaia ya Algeria katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Katika mchezo wa awali mabingwa hao walipoteza kwa goli 1-0 nchi Algeria na sasa Yanga inatakiwa kushinda ili kujiwekea mazingira mazuri yakusonga mbele.

Katika kundi hilo timu ya TP Mazembe inaongoza ikiwa na alama 10 ikifuatiwa na Medeama ambao wako sawa na Bejaia kwa pointi 5 wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa huku Yanga wakiburuza mkia.

Post a Comment

 
Top