BOIPLUS SPORTS BLOG

Karim Boimanda, Dar

MLINZI wa zamani wa Yanga, Rajab Zahir amejiunga na Wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Akizungumza na BOIPLUS, Afisa Habari wa klabu hiyo Dismas Ten alikiri kumalizana na mlinzi huyo ambaye Yanga walimpeleka kwa mkopo katika klabu ya Acacia Stand United kabla hajakwaruzana na kocha mkuu mfaransa Patrick Leiwig.

"Nipo kikaoni ndugu yangu lakini ni kweli amesaini mkataba utakaomuweka hapa kwa kipindi cha mwaka mmoja, " alisema Ten

City ilimsajili Juma Nyoso kama beki mzoefu lakini baadaye akafungiwa na shirikisho la soka TFF kwa utovu wa nidhamu hivyo kuacha pengo na sasa wameamua kusajili mzoefu mwingine kuongeza nguvu kikosini hapo.

Post a Comment

 
Top