BOIPLUS SPORTS BLOG

Bakari Kagoma, Dar
GOLIKIPA Saidi Kipao wa timu ya JKT Ruvu ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuchukua nafasi ya mlinda mlango Deogratius Munishi 'Dida' aliyefiwa na baba yake jana.

Stars imeingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria 'Super Eagles' katika mechi ya kukamilisha ratiba baada ya timu zote kushindwa kusonga mbele na kuwaacha Misri wakifuzu katika kundi hilo.

Kipa huyo alikuwa kwenye kiwango bora katika mchezo dhidi ya Simba uliochezwa Jumamosi iliyopita uwanja wa Taifa baada ya kuokoa michomo ya washambuliaji wa Wekundu hao waliokuwa wakiongozwa na Laudit Mavugo pamoja na Fredrick Blagnon kabla yakuingia kwa Ibrahim Ajib kipindi cha pili.

Ofisa Habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Alfred Lucas ameithibitisha BOIPLUS kuwa mlinda mlango huyo ameshajiunga kambini na wenzie tayari kwa safari ya kuelekea nchini Nigeria kwa mtanange huo.

"Ni kweli kocha wa timu ya Taifa Charles Boniface Mkwasa amemuita kikosi Kipao kuchukua nafasi ya Dida aliyefiwa na baba yake jana kwa ajili ya mchezo dhidi ya Nigeria," alisema Lucas.

Stars itashuka dimbani Septemba 3 jijini Lagos tayari kwa mtanange huo wa kulinda heshima.

Post a Comment

 
Top